UONGOZI WA CCM-TAIFA
Thursday, June 12, 2014
DKT ASHA MIGIRO AKUTANA NA BAN KI MOON, KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akiwa kwenye picha ya pamoja na Mh Dkt. Asha- Rose Migiro Waziri wa Sheria na Masuala ya Katiba ambaye yupo UN New York kuhudhuria Mkutano ulioitishwa na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu mchango wa Haki za Binadamu na Utawala wa Sheria katika Maendeleo Endelevu baada ya 2015.
Katika mazungumzo baina ya Mh Dkt Migiro na Bwana Ban Ki Moon, Katibu Mkuu alisema, Rais Jakaya Mrisho Kikwete amefanya jambo jema kumteua Dkt. Asha-Rose Migiro kwanza kuwa mbunge na kisha kumteua kuwa Waziri anayeshughulikia Sheria na Masuala ya Katiba, akasema uzoefu wake na mchango wake siyo tu kwamba ni muhimu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bali ni muhimu pia katika Jumuiya ya Kimataifa.
Ban Ki Moon alishindwa kuficha hisia zake pale aliposema mbele ya Maofisa wake kwamba siku zote amekuwa akimkumbuka Asha- Rose Migiro na kwamba amefurahi sana kwamba amepata nafasi yakufika Umoja wa Mataifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment