UONGOZI WA CCM-TAIFA

UONGOZI WA CCM-TAIFA

Thursday, June 12, 2014

DKT ASHA MIGIRO AKUTANA NA BAN KI MOON, KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akiwa kwenye picha ya pamoja na Mh Dkt. Asha- Rose Migiro Waziri wa Sheria na Masuala ya Katiba ambaye yupo UN New York kuhudhuria Mkutano ulioitishwa na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu mchango wa Haki za Binadamu na Utawala wa Sheria katika Maendeleo Endelevu baada ya 2015. 

Katika mazungumzo baina ya Mh Dkt Migiro na Bwana Ban Ki Moon, Katibu Mkuu alisema, Rais Jakaya Mrisho Kikwete amefanya jambo jema kumteua Dkt. Asha-Rose Migiro kwanza kuwa mbunge na kisha kumteua kuwa Waziri anayeshughulikia Sheria na Masuala ya Katiba, akasema uzoefu wake na mchango wake siyo tu kwamba ni muhimu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bali ni muhimu pia katika Jumuiya ya Kimataifa. 

Ban Ki Moon alishindwa kuficha hisia zake pale aliposema mbele ya Maofisa wake kwamba siku zote amekuwa akimkumbuka Asha- Rose Migiro na kwamba amefurahi sana kwamba amepata nafasi yakufika Umoja wa Mataifa.

Wednesday, June 11, 2014

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROF. MUHONGO APOKELEWA UBALOZINI DC

Waziri wa Nishati na Madini Prof. Muhongo akiwa kwenye picha ya pamoja na Mh Liberata Mulamula, Balozi wa Tanzania chini Marekana na Mexico baada ya kupokelewa ndani ya ofisi za ubalozi wa Tanzania huko Washington D.C.
Mh Muhongo yupo Marekani kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Afrika kuhusu nishati kwa wote.
CCM Tawi la Texas, tunamtakia makazi mema Mh Waziri na kumuomba siku nyingine afike kwenye Jimbo la Nishati la Texas hasa Jiji la Nishati la Houston.
Karibu sana Mh Waziri Marekani

Wednesday, June 4, 2014

TULIKOTOKA: SAID MTANDA MBUNGE WA CCM JIMBO LA MCHINGA

Mh. Said Mtanda, Mbunge wa Jimbo Mchinga kupitia CCM katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mh Mtanda ni mmoja kati ya wabunge vijana walioingia bungeni kwa mara ya kwanza katika uchaguzi wa mwaka 2010. Vilevile, Mh Mtanda ni Mbunge wa bunge la Afrika.
Tutamtafuta, siku za hivi karibuni tufanye nae mahojiano juu ya utekelezaji wa ilani ya CCM katika Jimbo la Mchinga. 

Tuesday, June 3, 2014

KINANA AKUTANA NA WACHIMBAJI WADOGOWADOGO WA MADINI, MERERANI


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akioneshwa vipande vya madini aina ya Tanzanite, katika mgodi wa mchimbaji mzawa wa madini ya Tanzanite Bi.Suzie Didas Kennedy. Katibu Mkuu wa CCM alitembelea migodi ya wachimbaji wadogo wa Mererani na kuzungumza nao juu ya changamoto zinazowakabili na namna ya kuzitatua. Pichani kati anayeshuhudia ni Mbunge wa Jimbo la Simanjiro, Mh. Christopher Ole Sendeka.
 Moja ya jiwe lenye madini kabla ya kufanyiwa mchakato. 
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia namna wachimbaji wadogo wanavyotumia mashine kubebea mchanga kutoka kwenye mgodi wa mchimbaji mzawa wa madini ya Tanzanite Bi.Suzie Didas Kennedy.Katibu Mkuu wa CCM alitembelea migodi ya wachimbaji wadogo wa Mererani na kuzungumza nao juu ya changamoto zinazowakabili na namna ya kuzitatua. 
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mererani ambao aliwaambia vyama vya Upinzania ni sawa na Jogoo kwani hata awike vipi hawezi fungua mlango na kwa sababu vyama hivyo havipo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi basi vinelekea kufa kwani havina sera mpya za kujinadi kwa wananchi. 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mererani wilaya ya Simanjiro ambao wengi ni wachimbaj wa wadogo wadogo wa madini kwenye mkutano wake wa mwisho baada ya kumaliza ziara ya siku 26 ambapo alitembelea mikoa mitatu ya Tabora, Singida na Manyara.