UONGOZI WA CCM-TAIFA

UONGOZI WA CCM-TAIFA

Tuesday, May 27, 2014

TUJIKUMBUSHE - MWENYEKITI WA CHADEMA APOKELEWA RASMI CCM


Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Mbeya Vijijini Bw Shintambala alipopokelwa rasmi CCM baada ya kuchoshwa na mizengwe ndani ya Chadema.

VIONGOZI WA CCM HUJENGWA HAWAOKOTWI BARABARANI

Mwenyekiti Mstaafu wa Umoja wa Wanawake wa CCM na Mbunge wa Viti Maalum Mama Anna Abdallah akimfunda Mh Angela Kairuki Naibu Waziri wa Sheria na Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa Wa Dar es Salaam. Mheshimiwa Angela ni moja ya matunda ya kazi nzuri ya UWT.

Friday, May 16, 2014

MADIWANI WA CUF WILAYANI URAMBO WASHIRIKI MAPOKEZI YA KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA NA UJUMBE WAKE



 Madiwani wa Chama cha CUF,wilayani Urambo wakimpokea kwa bashasha kubwa katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwasili katika wilaya ya Urambo,mapema leo akitokea wilayani Sikonge.Shoto ni Diwani wa CUF,Mh.Kandola Nyanda wa kata ya Nsenda na kati ni Diwani wa CUF,Kata ya Usoke,Mh.Kadada Mohamed,ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya elimu,afya na maji katika halmashauri ya Urambo mkoani Tabora.Pichani nyuma ya Kinana ni Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye akifurahia jambo.
Diwani wa CUF,Mh.Kandola Nyanda wa kata ya Nsenda akimpokea kwa bashasha kubwa katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwasili katika wilaya ya Urambo,mapema leo akitokea wilayani Sikonge.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Mh Fatma Mwasa akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Urambo,Mh.Samwel Sitta mara baada ya kuwasili kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana Wilayani Urambo mapema leo.
 Mbunge wa Urambo Mashariki Mh.Samwel Sitta akimkaribisha katika jimbo lake Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake mapema leo.
 Katibu Mkuu wa CCM ,Ndugu Kinana akizungumza jambo na Mbunge wa Urambo Mashariki Mh.Samwel Sitta,Pichani kati ni Mkuu wa Mkoa,Mh.Fatma Mwasa pamoja na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye.
  Katibu Mkuu wa CCM ,Ndugu Kinana pamoja na Mbunge wa Urambo Mashariki Mh.Samwel Sitta wakishiriki ujenzi wa jengo la maabara katika shule ya sekondari Uyumbu,katika kata ya Uyumbu wilayani Urambo mkoani Tabora

Tuesday, May 13, 2014

KAMATI KUU YA CCM YAMFUNGA MDOMO SITTA

Samuel Sitta
Maamuzi ya Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kukakataa uwezekano wowote wa kufanyika kwa mazungumzo ama baina yake au kiongozi yeyote wa serikali na Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi (Ukawa), umevunja juhudi za Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta, kutaka kukutana na umoja huo kwa mazungumzo.
Chama hicho kupitia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, jana kilitangaza rasmi mjini hapa kwamba hakina mpango wa kuzungumza au kuishawishi serikali au viongozi wake kutafuta ufumbuzi ili Ukawa warejee bungeni.

Nape alitoa msimamo baada ya kumalizika kwa kikao cha dharura cha Kamati Kuu (CC) ya chama hicho kilichofanyika juzi chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.

Alisema hakuna sababu ya kuendelea kuwabembeleza Ukawa na kwamba watapingana nao na kuwashughulikia huko huko kwa wananchi wanapokwenda.

Baada ya Ukawa unaoundwa na wabunge wa Bunge Maalum la Katiba kutoka Chadema, Cuf na NCCR-Mageuzi, kutoka bungeni Aprili 16, mwaka huu wakituhumu wajumbe wa CCM kwa ubaguzi, kejeli na uchakachuaji wa Rasimu ya Katiba, Aprili 21, mwaka huu Sitta alianza juhudi za kukutana nao nje ya Bunge, lakini hakufanikiwa licha ya kukutana na Katibu Mkuu wa Cuf, Maalim Seif Sharif Hamad ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.